Episode's summary
Musharraf al-Din Mosleh ibn Abdullah ibn Musharraf, ambaye baadaye alijulikana kama Saadi Shirazi, ni mmoja kati ya malenga na mshairi mkubwa na mashuhuri nchini Iran. Wanahistoria wanaamini kwamba Saadi Shirazi alizaliwa kati ya mwaka 600 na 610 Hijiria (sawa na takriban mwaka 1210 Miladia). Walakini, hakuna tarehe kamili inayojulikana ya kuzaliwa kwa malenga huyu, ingawa wanahistoria wanakadiria mwaka huo wa kuzaliwa kulingana na athari za kazi zake. Saadi alizaliwa katika familia ya wanazuoni, wasomi na watu wenye maadili mema. Baba yake alikuwa mfanyakazi wa Mahakama ya Atabak na Shah Saad bin Zangi. Wengine wanaamini kwamba mshairi huyu amechagua jina la ukoo la Saadi kama ni mtu mwenye utambuzi wa haki. Mbali na kuhudumu katika mahakama, baba yake pia alikuwa akijishughulisha na masuala ya kidini na alikuwa akimshajiisha mno mtoto wake kujifundisha elimu ya kisekula na kidini pia. Kwa msaada wa baba yake, Saadi alipata ujuzi wa kina katika nyanja za historia na fasihi. Wakati wa kuzaliwa kwake, mtawala…
Musharraf al-Din Mosleh ibn Abdullah ibn Musharraf, ambaye baadaye alijulikana kama Saadi Shirazi, ni mmoja kati ya malenga na mshairi mkubwa na mashuhuri nchini Iran. Wanahistoria wanaamini kwamba Saadi Shirazi alizaliwa kati ya mwaka 600 na 610 Hijiria (sawa na takriban mwaka 1210 Miladia). Walakini, hakuna tarehe kamili inayojulikana ya kuzaliwa kwa malenga huyu, ingawa wanahistoria wanakadiria mwaka huo wa kuzaliwa kulingana na athari za kazi zake. Saadi alizaliwa katika familia ya wanazuoni, wasomi na watu wenye maadili mema. Baba yake alikuwa mfanyakazi wa Mahakama ya Atabak na Shah Saad bin Zangi. Wengine wanaamini kwamba mshairi huyu amechagua jina la ukoo la Saadi kama ni mtu mwenye utambuzi wa haki. Mbali na kuhudumu katika mahakama, baba yake pia alikuwa akijishughulisha na masuala ya kidini na alikuwa akimshajiisha mno mtoto wake kujifundisha elimu ya kisekula na kidini pia. Kwa msaada wa baba yake, Saadi alipata ujuzi wa kina katika nyanja za historia na fasihi. Wakati wa kuzaliwa kwake, mtawala…
Episodes
MALENGA WA KIIRANI SAADI SHIRAZI
ListenedMusharraf al-Din Mosleh ibn Abdullah ibn Musharraf, ambaye baadaye alijulikana kama Saadi Shirazi, ni mmoja kati ya malenga na mshairi mkubwa na mashuhuri nchini Iran. Wanahistoria wanaamini kwamba Saadi Shirazi alizaliwa kati ya mwaka 600 na 610 Hijiria (sawa na takriban mwaka 1210 Miladia). Walakini, hakuna tarehe kamili inayojulikana ya kuzaliwa kwa malenga huyu, ingawa wanahistoria wanakadiria mwaka huo wa kuzaliwa kulingana na athari za kazi zake. Saadi alizaliwa katika familia ya wanazuoni, wasomi na watu wenye maadili mema. Baba yake alikuwa mfanyakazi wa Mahakama ya Atabak na Shah Saad bin Zangi. Wengine wanaamini kwamba mshairi huyu amechagua jina la ukoo la Saadi kama ni mtu mwenye utambuzi wa haki. Mbali na kuhudumu katika mahakama, baba yake pia alikuwa akijishughulisha na masuala ya kidini na alikuwa akimshajiisha mno mtoto wake kujifundisha elimu ya kisekula na kidini pia. Kwa msaada wa baba yake, Saadi alipata ujuzi wa kina katika nyanja za historia na fasihi. Wakati wa kuzaliwa kwake, mtawala…
ATTAR NEYSHABURI MALENGA WA KIIRANI
ListenedATTAR NEYSHABURI MALENGA WA KIIRANI Tarehe 25 Farvardin kwa mujibu wa ( Kalenda ya Kiirani) inayosadifiana na tarehe 14 Aprili, ni siku ya kumkumbuka na kumuadhimisha malenga wa Kiirani Farid al-Din Abu Hamid Muhammad bin Abu Bakr Ibrahim bin Is- haq Attar Neyshabouri, ambaye ni mmoja wa washairi mashuhuri, aaref na mwanafikra mkubwa wa Kiirani aliyeishi mwishoni mwa karne ya sita na mwanzoni mwa karne ya saba Hijria. Baadhi ya wanahistoria wameandika kuwa, mwanafikra na malenga huyo wa Kiajemi amezaliwa mwaka 513 na wengine wanaeleza kuwa alizaliwa mwaka 537 Hijiria. Attar Neyshabouri alizaliwa katika kijiji cha Kadkan au Shadiakh, ambacho wakati huo kilikuwa sehemu ya jiji la Neyshabour. Hakuna habari inayoelezea taarifa zake za utotoni mwake, isipokuwa baba yake aliishi katika mji wa Shadiakh akifanya kazi ya kuuza dawa za asili, na alikuwa mahiri na hodari mno katika biashara hii ya kuuza dawa za asili, na baada ya kufariki dunia baba yake, Farid al Din Attar Neyshabouri aliendeleza shughuli za marehemu…
Siku kuu ya Nowruz Mwaka Mpya wa Kiiran
ListenedJumatatu ya Tarehe 21 Machi 2022 Miladia inayosadifiana na tarehe (Mosi / Farvardin 1401) ni siku ya kuanza mwaka mpya wa Kiirani wa Hijria Shamsia. Siku hii ambayo hujulikana kama Nowruz, ni mwanzo wa sherehe za kale na za muda mrefu na matawi yake yameenea katika kona mbalimbali za Dunia hadi Afrika Mashariki. Asili ya sherehe za Mwaka Kogwa huko Makunduchi visiwani Zanzibar, ni sherehe hizo za Nowruzi za nchini Iran.
Mwanamalenga wa Kiirani Nezami
ListenedJamaluddin Abu Mohammad hakuweza kupata upendo wa wazazi wake kwa muda mrefu; kwani wazazi wake walifariki dunia akiwa bado mtoto na kupata malezi akiwa mtoto yatima. Ushahidi wa kihistoria unaonyesha kuwa, Nezami Ganjavi hakuwahi kuondoka katika mji wa Ganja akiwa bado na umri mdogo, na alipofikia marika ya ujana , aliweza kujifunza sanaa na ujuzi mbalimbali na hatimaye alikuwa na ufasaha wa kuzungumza na kuandika lugha za Kiazeri, Kiarabu, Kiajemi na Kipahlavi. Nezami ni bingwa na mshairi anayepaswa kuzingatiwa kwenye mihimili na nguzo za ushairi wa Kiajemi. Yeye ni mmoja wa malenga aliyekuwa na kipaji cha kuandika mashairi na kuyasoma kwa sauti nzuri, iliyowavutia wasikilizaji. Ingawa hekaya na simulizi za hadithi za Kiajemi hazikuanzishwa na Nezami, lakini gwiji huyo anahesabiwa kuwa ni mshairi pekee aliyeweza kuendeleza ushairi wa mafumbo kwa kiwango cha juu zaidi kufikia mwisho wa karne ya sita. Nezami aliweza kujiwekea nafasi maalumu katika fasihi ya lugha ya Kifarsi inayotumika Iran na ametumia…
Kumbukizi ya Miaka miwili ya Luteni Jenerali Qassem Suleimani 3 January 2020
Listenedkumbukizi ya miaka 2 ya shujaa mpigania haki na amani Haj Qassem Suleimani, ambapo aliuiliwa Shahidi na Majeshi dhalimu ya Marekeni mjiini Baghdad nchini Iraq. Kamanda Soleimani ambaye amepewa lakabu ya bwana wa mashahidi wa muqawama, katika umri wake wote uliojaa baraka na akiwa kamanda wa IRGC, alikuwa mstari wa mbele kuyasaidia na kuyaunga mkono mataifa yote yanayodhulumiwa ya Waislamu, bila ya kujali ni mataifa ya watu gani. Muhimu kwake muda wote ilikuwa ni kupigania Uislamu na mafundisho sahihi ya Qur'ani Tukufu. Shujaa huyu (Qassem Soleimani) alizaliwa tarehe 11 Machi 1957, katika kijiji cha Qanat-e Malek, Mkoa wa Kerman nchini Iran. Baada ya kumaliza masomo akiwa na umri wa miaka 18, alihamia mjini Kerman na huko aliajiriwa na Shirika la Maji la mji huo. Wakati wa harakati za mapinduzi ya Kiislamu zikiwa zimepamba moto, Qassem Soleimani alifahamiana na mwanachuoni mmoja wa kidini aliyeitwa Sheikh Reza Kamyab aliyetoka mji wa Mashhad, ulioko kaskazini mashariki mwa Iran na kwenda mjini Kerman…